X Plastaz

Nini Dhambi Kwa Mwenye Dhiki? Songtext / Lyric


X Plastaz - Nini Dhambi Kwa Mwenye Dhiki? Songtext


All my people

East Africa

Tanzania, Uganda and Kenya

Dar es Salaam, A town

Wherever you are

Piga magoti, tuombe Mungu Hii ni siasa, dini, vita, ubwana,

utwana, au kiama ghalika,

sodoma na gomora?

Simama imara, zunguka kila

kona, kila anga angaza

Kushoto, kulia, mbele, nyuma kote pitia



Na hapo ulipojishikiza

g'ang'ania, sikilizia, vumilia

baadae usije jutia Hii ni mahususi na maalum

kwa watu wangu

Walemavu, vipofu, zeruzeru na

wendawazimu

Watoto wa mitaani, fukara,

masikini na wenye akili zao timamu






Hii kamba ngumu

Mjue tunavutana na wenye

nguvu

Vitambi na mashavu

Hakuna tena fair game Refarii kauzu

Uwanja wenyewe mkavu

Ujira mgumu, malipo finyu

Kilichobaki kucheza rafu

Tumechoshwa na ukabaila,

ubepari na ubeberu



Wakati ndo huu

Ukombozi ndo huu

Na sasa naamuru mliopo chini

wote mpate divai ya vinibu

Mtetezi wenu nikaze gidamu



Nimwage sumu ya ----- juu yao

Wajikune bila aibu

Kwanza saluti kwa

waliyotangulia kuzimu

Pili tuombe Mungu

Baba yetu, utupe mkate wetu wa kila siku

Utujaze nguvu

Tupate kudumu ndani ya game

Tutakapofika kuzimu siku ya

hukumu

Utupe nafasi tupate kutubu Kwani tunajua tunatenda

maovu

Tunakula haramu

Tunatumia kila mbinu

Juju, uhalifu, upanganyifu

Ili tuweze kujikimu Lakini isiwe kisingizio kwa

wanadamu wengine

kunyimwa haki zetu

Kutuzibia riziki zetu

Kutuita makafiri, dharau na

kutukashifu Kwani nini dhambi



Nini dhambi kwa mwenye

dhiki,

Kipi haram, kipi halali,

Kila mmoja anaitaka hii riziki

Kitendawili, vurugu mechi Huwezi tabiri Kwa nini?



Uliza swali, kama

sote tungekuwa wasomi,

matajiri

Ni nani angelifanya kazi za

kutisha na hatari mfano ya

mochwari Kila mmoja wetu hapa mjini

kaja kwa dili

Kila kitu, kila mahali

Na hata ngozi ya mtu dili

Wengine wachawi, waganga

feki Matapeli, wasafiri ------

Wakati wengine wapole kama

walokole



Mchana pirika nyingi maofisini

Kumbe night kali, kahaba

Shuga, jambazi, mengine ya kusitiri

Ah!

Wapo waliopoteza maisha

katika kufight life

Kumbukumbu zao zimebaki

makaburini Na wapo waliopoteza kabisa

tumaini la kuwini

Hao roho zao utadhani

wamezitoa rehani

Wakikutight mahali fulani

Inabidi uwakabidhi mshahara wote wa mwisho wa mwezi



()



Kweli Bongo kutafuta braza

Utajajuta utakapojikuta huna

hata bukta

Shauri yako we tegesha tu

kama golikipa

Na hao unaowategemea mwishowe watakutosa

Huna elimu, hun fani

Lakini nguvu, hulimi, uchumi

unao unaukalia

Kumbuka

Kupata au kukosa yote ni kawaida

Sometimes unalala unaota

unakula

Unakunywa, unapiga denda

Na kula uroda na demu bomba

Ukikurupuka tu unakuta patupu

Hakuna kitu



(, Yamat singing a

traditional Maasai song)

Dieser Songtext wurde von www.Deine-Songtexte.com heruntergeladen :)

"Nini Dhambi Kwa Mwenye Dhiki?" Video ansehen

Was denkst du über "Nini Dhambi Kwa Mwenye Dhiki?"?